GET /api/v0.1/hansard/entries/1157920/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1157920,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1157920/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuunga mkono Mswada huu. Bunge la Taifa liko na majukumu ya kuangazia sheria zilizoko na zile ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho zinafanyawiwa marekebisho wakati wowote. Mwenzangu Mhe. Sankok amesema kwamba tunapoelekea uchaguzi sio wakati mwafaka wa kubadilisha sheria za uchaguzi. Mawazo hayo sio sawa. Tuko na vikao mpaka mwezi wa sita. Hata kama kutabaki siku moja kusitisha vikao vyetu na uchaguzi utakuwa umebakia miezi miwili, kama kuna jambo litakalokuja katika mawazo ama katika Bunge la Taifa ambalo litawezesha uchaguzi ufanyike katika hali ambayo ni shwari zaidi na itakayokuwa ya wazi zaidi, basi itakuwa sawa kufanya marekebisho hayo."
}