GET /api/v0.1/hansard/entries/1157925/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1157925,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1157925/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "Pili, sheria hii inasema kwa urahisi kwamba ukitaka kujitambulisha kama mpiga kura, basi unahitaji kitambulisho ama passport ambayo iko sawa. Hili ni jambo zuri. Kulikuwa na wasiwasi ama taharuki Kenya nzima. Watu wengine walidhani kwamba Huduma Namba zitatumika ndio upige kura. Sheria hii inafanya mambo haya kuwa wazi. Lakini wakipiga kura tunakuwa na changamoto sana na rufaa. Mtu ambaye hajaridhika kama Mjumbe wa Bunge la Kaunti akilalamika kortini, mambo haya yanachukua muda mrefu sana. Ni lazima iende tena mpaka kwa korti ya juu. Lakini leo hii, sheria hii inaeleza kwa urahisi kwamba mtu ambaye anawania kiti cha wodi ama Bunge la Kaunti akiwa na malalamishi baada ya uchaguzi, basi maamuzi yale yatafanywa katika korti ya chini. Hili ni suala nzuri. Hii inamaanisha kwamba mambo haya yatasuluhishwa kwa urahisi. Mahakama ya juu itabaki kuangalia yale malalamishi ya wale ambao hawataridhika kutoka ngazi ya kitaifa ambapo ni Mbunge na kwenda juu."
}