GET /api/v0.1/hansard/entries/1158280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1158280,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1158280/?format=api",
    "text_counter": 138,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bi. Spika wa Muda. Pia mimi nataka kumpa kongole Sen. (Dr.) Kang’ata, Senator mchapa kazi kutoka Kaunti ya Murang’a kwa kuleta Hoja hii hapa. Sen. (Dr.) Kang’ata saa ingine hucheka tu hata jambo sio la kuchekesha. Sijui ni binadamu wa aina gani lakini nafikiria kwa sababu hiyo, watu wa Kaunti ya Murang’a wakampenda sana. Bi. Spika wa Muda, swali hili la kwa nini Kenya haina petroli si swala la kulaumu mtu mmoja. Sen. (Dr.) Kang’ata katika uwezo wake amekuwa akiongea hapa ndani ya Seneti hususan akimlaumu Rais zaidi na serikali yake. Mimi nashangaa sana siku hizi amekuwa kama kinyonga. Kinyonga hugeuka rangi. Yeye wakati ule alikuwa anapiga siasa hapa, hatujaona mtu aliyekuwa akisifu Rais ndani ya sii Seneti kushinda Sen. (Dr.) Kang’ata. Leo amepinduka amekuwa kinyonga sasa amekuja katika rangi ya kumtukana na kumpinga Rais kwa maneno ambayo hayafai. Lazima afanye heshima kwa sababu hata"
}