GET /api/v0.1/hansard/entries/1158282/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1158282,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1158282/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "kule kwao nyumbani anakotoka, ukiwa umezidi mtu na umri, hata kama mmekosana, unaweza kusema mambo utakayosema lakini lazima uweke mpaka kama heshima wa jamhuri ya Kenya. Ndio sababu kule wako na jina wanaita mutongoria. Kama yeye hawezi kuheshimu mutongoria kutoka kwao, je watu wengine katika Kenya watafanyaje? Bi. Spika wa Muda, ni ukweli kabisa kwamba Kenya sasa petroli haipatikani. Hii imesababishwa na ufisadi. Ufisadi lazima uangaliwe vizuri kwa sababu kama ni ugonjwa umeingia, kama ni COVID-19, kila mtu hapa anajikinga. Hivi ni vita dhidi ya ufisadi. Ndani ya serikali, kuna watu ambao wametufikisha katika hii level ambayo sisi hatuwezi kukubali tena. Ikiwa wewe ni mwizi au mtu ambaye anafanya vitu ambavyo havifai na kila mtu katika Kenya anavikemea wewe umetuleta mpaka tumefika tulipo. P ia mimi nasema, hata ikiwa sisi tuko hapa kama Wakenya, sote tukiwa tunaumia na baa la njaa, tunaumia na ugonjwa wa aina flani na maradhi haya yameletwa na ufisadi, basi afadhali. Kule nyumbani tunasema mganga anayetibu jipu wakati akiwa anakutibu, unaumia, lakini wakati hilo jipu limepoa, ametoa ule moyo, unaona ya kwamba kila mtu anastarehe na anashukuru kwa sababu mganga amefanya kazi yake. Bi. Spika wa Muda, ni sababu hii nasema ya kwamba ni lazima Rais achukue kiboko sasa. Kama kuna Waziri na Katibu Mkuu ambaye ameweza kuleta hii Serikali ama nchi kwa hali ambayo tuko sasa, ni lazima hatua ichukuliwe. Nataka kuona Rais akichukua kiboko akichapa wale wote wanahusikana na mambo ya ufisadi. Bi. Spika wa Muda, tunajua katika utengezaji chakula, kama mtatengeza mafuta, wale wapandaji mahindi ambao ni wakulima wnatumia jenereta katika maeneno ambayo hayana umeme. Vile vile kama ni upande wa usafiri, watu wanapokwenda kazini au katika hospitali, kuna hospitali ambazo ziko katika maeneo ambayo hayana stima na zinatumia jenereta ambayo inatumia dizeli. Kuna wagonjwa kule ambao wanategemea hewa ya oksijeni kupitishwa kutoka kwa ile ambayo itatumika katika jenereta ili kusambazwa na watu waendelee kuwa na maisha mema. Sasa wakulima hawawezi kuenda shambani na matingatinga yao. Watu hospitalini watakufa kwa sababu katika zile hospitali ambazo jenereta haifanyi kazi kwa sababu hakuna petroli. Watu wanaofanya kazi mbali hawawezi kutoka asubuhi kwa sababu hakuna Matatu. Wataenda namna gani kazini? Mtu akichelewa atafutwa kazi; asipoenda ndio balaa zaidi. Hii ni janga. Lazima Rais aangalie na achukue hatua. Mambo ya kulaumiana kwamba Rais hafanyi hivi, Rais hafanyi vile tungeweka nyuma kwanza. Tuangalie hili janga kwanza mpaka liweze kupita tuliweke nyuma. Bi. Spika wa Muda, nataka kukubaliana sababu zote ambazo zimetolewa. Kwa sababy hakuna petroli ndani ya nchi hii, kama ni mtihani, ningesema Rais Uhuru Kenyatta ameanguka mtihani. Haya ni kwa kuwa sababu alizotupatia sisi kwa nini hakuna petroli hazifui dafu hata kidogo. Kwa hivyo, tunasema ya kwamba ni ukweli anakumbwa ama amezungukwa na watu ambao ni wezi na watu ambao hawafai katika yale mamlaka. Ni lazima achukue hatua. Bi. Spika wa Muda, la mwisho. Kiongozi wa Walio Wengi umempatia dakika tano. Naomba nipate dakika tatu tu."
}