GET /api/v0.1/hansard/entries/1158285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1158285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1158285/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, asante. Jana nilikuwa katika safari yangu ya kutoka mashinani nikija huku. Ni ukweli kabisa alichosema ndugu yangu Sen. Wetangula. Katika kila kituo ambapowanauza petroli, wananchi wenye Boda boda wamejaa. Kwanza, wamejaa na majonzi kwamba hakuna petrol. Pili, wamejaa kwa sababu wale Boda boda wanakula kila siku kulingana na ile pikipiki. Wenye pikipiki wanasema ya kwamba hawataki kuchukua kitu kidogo kuliko kile wanachukua kila siku. Ukiwa umekodisha pikipiki kufanyia kazi, ni umpatie ule mtu ile pesa ambayo inatakikana kwa ile pikipiki kwa siku moja. Saa hizi, utapata Boda boda wenyewe hata kupeleka watu haiwezekani. Umaskini umekithiri ndani ya nyumba za watu kama Boda boda, mama mboga na kila sehemu za sekta ambazo ni za uchumi. Sisi tunasema ya kwamba, katika ile hali ambayo iko hivi sasa, ni bora tufike katika kikomo. Tunasema ya kwamba Rais hivi sasa, si lazima ya kwamba sote tupige kelele ya kwamba ajiondoe katika mamlaka. Tunasema kitu kimoja, Rais ni lazima achukue hatua mwafaka ambayo itakuwa suluhisho na onyo kwa wale ambao wana tabia zile wanafanya katika ofisi mpaka wamefikisha milioni arubaini ya Wakenya pale tulipo hivi sasa."
}