GET /api/v0.1/hansard/entries/1158305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1158305,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1158305/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Wakenya wamekumbwa na majanga mengi, likiwemo janga la korona na ukame. Leo hii kuna uhaba wa mafuta nchini. Nilisafiri juzi. Nilikuwa miongoni mwa watu waliopanga foleni ndefu kusubiri mafuta. Kule nitokako, wale wanaoathirika zaidi ni watu wanaondesha boda boda. Bi. Spika wa Muda, kwa kweli, Hoja hii imefika wakati mwafaka. Sen. Kang’ata ameleta Hoja hii wakati unaofaa kwa sababu hili ni janga ambalo limetukumba. Endapo ulipata muda wa kutembea katika sehemu za Nairobi, katika vituo vya kuuza mafuta, mtu alikuwa anawekewa mafuta ya Ksh1,000 pekee ili watu wengine waweze kupata mafuta. Hakuna haja ya kumlaumu Rais wa nchi hii. Rais anajua kuwa lawama zote zinaelekezwa kwake. Siwezi kusita kusema kwamba Rais amezingirwa na watu ambao wanamvuta nyuma. Ni lazima tuseme hayo katika Seneti kwa sababu kama wezi wamekuzingira, basi wamekuzingira. Anafaa kujua kuwa lawama zote zinaelekezwa kwake. La muhimu ni kufanya kazi ili kuepukana na balaa. Ni vyema kutafuta suluhu ili kuwakikishia kuwa shida kama tuliyonayo hairudi tena. Rais alitia sahihi Mswada juu ya bajeti ya ziada inayopendekeza kutenga Ksh34 billion ili tuweze kupata mafuta kwa urahisi. Sehemu ambazo sisi tunatoka hazijaendelea. Katika maeneo mengi, watu wanatumia jenereta ambazo huhitaji mafuta. Kama hospitali inatumia jenereta na mafuta ikosekane, kunaweza kutokea janga kubwa kwa sababu operesheni haiwezi kufanyika kwa sababu ya ukosefu wa mafuta. Katika sehemu zingine ambazo baadhi yetu tunatoka, baadhi ya watu hutumia mafuta kuzalisha umeme. Hii imechangia hali kudorora na kuathiri maisha ya Wakenya katika sehemu hizo."
}