GET /api/v0.1/hansard/entries/1158796/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1158796,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1158796/?format=api",
    "text_counter": 36,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, najiunga na wewe mchana wa leo kwa kuwakaribisha wale wangwana ambao ni wafanyikazi katika Kaunti ya Machakos. Kwanza, nawakaribisha na kuwaambia kwamba hapa ndipo kuna kina cha maelezo au ujuzi wote mnahitaji kuijua. Kuja kwenu hapa, mtatoka mkiwa mmeelimika kisawasawa. Ninatumaini ya kwamba yale yote ambayo mmejifundisha yataenda kwa muda mrefu sana kusaidia watu wa Kaunti ya Machakos. Cha mwisho ni kwamba nawapa kongole watu wa Machakos kwa kuonyesha mfano wa kwamba mwanamke pia anaweza kuchaguliwa akawa kiongozi. Nasema mwanamke kwa sababu ni jinsia ya maumbile ya binadamu. Mama Kavindu kama tunavyoelewa hapa ndani ya Seneti ni mama shupavu. Ni Seneta ambaye anajihusisha katika kila hali. Kila akiwa hapa, cha muhimu ni kwamba yeye huwa anaongea mambo ya Machakos kisawasawa na kutetea Kaunti yake ya Machakos. Kwa hivyo, mlifanya vizuri sana kumchagua mama shupavu ambaye anaweza kuwawakilisha katika Bunge la Seneti kisawasawa"
}