GET /api/v0.1/hansard/entries/1160755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1160755,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160755/?format=api",
    "text_counter": 21,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii nitume risala zangu za rambirambi kwa ndugu zetu kwa kumpoteza Spika. Sisi kama Jumuia ya Afrika Mashariki, ni jambo ambalo limetupiga na kutuacha na mshangao. Huyu ni mtu ambaye tulimjua kama aliyejitolea mhanga na kufanya kazi yake huku akizingatia sheria. Siku ya leo, ninaleta risala zangu mwenyewe, familia yangu na za watu wote wa Kaunti ya Laikipia. Tungependa kuwaambia ndugu zetu wamtegemee Mwenyezi Mungu kwa sababu hakuna jambo ambalo linatendeka bila Mwenyezi Mungu kujua, ikiwa ameketi katika Kiti chake cha Enzi. Mimi mwenyewe sikuwa nimekutana naye, lakini ninajua Bi Naibu Spika na wengine walijumuika naye katika shughuli tofauti. Mimi kama Seneta wa Laikipia nasema pole. Tunatuma pole zetu kwa ndugu zetu na kuwaambia ya kwamba hili ni jambo ambalo limetuacha na kiwewe. Tutawaombea Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi na wakati wa kiama utakapofika, aweze kukumbukwa. Mambo aliyoyafanya katika inchi yake yataandikwa kwa wino usiofutika katika daftari ambazo hazitasahaulika. Mswahili husema mghala muue na haki mpe. Ametenda wema na wema utamfuata. Tunawaambia familia yake pole. Mambo aliyotenda katika inchi yake yakumbukwe na yawe mfano wa kuigwa. Hata Jamhuri yetu ya Kenya pamoja na Afrika nzima iige mfano wake kwa sababu ni mtu ambaye alifanya kazi kwa kujitolea. Bi. Naibu wa Spika, asante kwa nafasi hii. Ninaomba nikomee hapo ndio niwape fursa wenzangu ambao wangependa kuchangia. Ndiposa tuimarishe lugha yetu ya Kiswahili, ningeliomba hata ndugu zangu watakaochangia siku ya leo, wajifunge kibwebwe na kuchangia kwa Kiswahili. Hivyo ndivyo tutakavyoweza kufanikisha lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki, Afrika kwa jumla na hata duniani kote."
}