GET /api/v0.1/hansard/entries/1160771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1160771,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160771/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Mkiketi naye hauwezi fikiria kuwa wakati unaenda. Baada ya muda, ndipo utaona saa zimeenda maana mkiwa naye, mnakula mkicheka na kuzungumza. Kwa hivyo, ni jambo la kusikitisha sana kwamba alipatatikana na ugonjwa wa saratani ambao haukugunduliwa mapema na hivi sasa umechukua maisha yake ilhali umri wake haukua mkubwa sana."
}