GET /api/v0.1/hansard/entries/1160781/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160781,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160781/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Orengo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 129,
"legal_name": "Aggrey James Orengo",
"slug": "james-orengo"
},
"content": " Asante sana Bw. Spika wa Muda. Nami pia najiunga na Maseneta wenzangu kutuma risala zangu za rambirambi. Si zangu tu, bali pia kwa niaba ya wakaazi wa Siaya na wananachi wa Kenya kwa jumla. Sisi sote tunatoa risala zetu za rambirambi kwa wananchi wa Uganda. Sikumjua Spika Oulanyah kwa kibinafsi. Lakini, nimesoma na kujua kumhusu. Kwa kweli ukijua historia ya Uganda, imepitia pahali pagumu kisiasa. Najua mwenzangu, Kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti, Sen. Poghisio, anafahamu historia hiyo kuliko wengi katika Seneti na wanasiasa kwa jumla."
}