GET /api/v0.1/hansard/entries/1160782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1160782,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160782/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": "Nimesoma na nimepata kujua kwamba mwenzetu, Spika Oulanyah, alifanya kazi muhimu katika kupitisha marekebisho ya katiba Uganda. Marekebisho ya Katiba ya Uganda hayakuwa rahisi. Nchi ya Uganda imekuwa na historia ngumu zaidi ukilinganisha na historia yetu ya kisiasa kwa sababu iliwahi kuongozwa na serikali ya kijeshi. Mawakili na wanasiasa kama yeye walijitokeza kuona kwamba kuna uongozi wa kidemokrasia Uganda. Pongezi kwake. Wakati watu watafikiria kuandika – hata pengine historia ya Uganda ishaandikwa – kutakuwa na sehemu kubwa ya aliyekuwa Spika Mhesh. Oulanyah kuonyesha vile alitetea uongozi wa kidemokrasia na Katiba ambayo ilipitishwa akiwa katika Bunge la Uganda. Kwa kweli, wadhifa wa Spika katika nchi yoyote ya kidemokrasia ni muhimu sana. Wakati mwingine hatufikirii kwamba wadhifa wa Spika ni muhimu. Kuna baadhi ya Maseneta hapa ambao wameona kuwa wadhifa wa Spika si rahisi."
}