GET /api/v0.1/hansard/entries/1160784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1160784,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160784/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": "Wakati Chief Justice wa kwanza alipoteuliwa, kulikuwa na hali ngumu ya kisiasa katika nchi ya Uganda. Kuna wakati Chief Justice Kiwanuka na Wabunge walijaribu sana kuona kwamba Uganda inalinda Katiba na kuzingatia demokrasia lakini hawakufaulu kwa sababu baadaye Jemedari Amin alichukua uongozi na kurekebisha hali hiyo. Hatimaye kulikuwa na vita. Watu waliuwawa, wengine walikamatiwa na wengine walitoroka Uganda. Kwa hivyo, nampongeza sana aliyekuwa Spika kwa sababu katika hali hiyo ngumu, yeye pamoja na wanasiasa wengine wa Uganda walijaribu sana kuona kwamba kuna serikali ya kidemokrasia katika nchi ya Uganda. Nafikiri wakati huu ambapo tunataka--- Tutakuwa na uchaguizi mwaka huu. Tatachagua Wabunge katika Bunge la Kitaifa na Seneti. Tutakuwa na Wabunge wa kuchaguwa Maspika katika Mabunge yetu mawili; Seneti na Bunge la Kitaifa. Wanafaa kuwa washupavu wa kuchagua watu wenye msimamo kama aliyekuwa Spika wa Uganda Hon. Jacob Oulanyah. Kwa hayo machache, Bw. Spika wa Muda, nikubalie tena nitoe risala zangu za rambirambi. Asante sana."
}