GET /api/v0.1/hansard/entries/1160786/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1160786,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160786/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii, kwa niaba ya wakaaji wa Kaunti ya Kericho ambao ninawakilisha katika Bunge hili, kutoa rambirambi zangu binafsi, jamii yangu, na wao kwa jumla, kwa Bunge na taifa la Uganda kwa kumpoteza Spika wao. Kama vile mmoja wetu alivyosema, mwaka uliopita mwezi wa Disemba, tulipata fursa ya kujumuika naye katika michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha. Ingawa hatukuzungumza kwa ukaribu, tulipata kushabikia timu zetu pamoja. Tulifurahia kwa wiki mbili ambapo michezo hiyo ilifanyika. Kulingana na vile nilivyomwona wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake kama Spika na kuongoza timu za Uganda katika michezo, alikuwa mtu mkakamavu aliyependa watu na uongozi wake uliheshimika na Wabunge wa Tanzania. Mabunge ya Afrika Mashariki yanatambuana kwa sababu tunalenga kuleta uwiano. Tuna matumaini kwamba siku moja tutaweza kufikia ndoto yetu ya kupata maazimio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuwa watu wamoja, kwa kuzungumza lugha moja na katika kazi zetu. Tunatarajia kuwa mazungumzo ya simu yatatozwa ada sawa katika mipaka yetu. Watu wasiwe wanaitishwa vitambulisho kwa sababu sisi wote ni ndugu na dada. Hatuwezi kuyapata hayo kama hatutachukua fursa kutambuana na kusimama na wenzetu wakati wa janga kama hili. Ni vyema kwamba Bunge la Kenya limechukuwa muda huu wote kupeana pole na rambirambi zetu kwa watu wa Uganda ili wajue sisi tunawapenda, tunawaheshimu na tunawaona kama ndugu. Kwa niaba ya watu wa Kericho, ninatoa rambirambi zetu."
}