GET /api/v0.1/hansard/entries/1160790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160790,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160790/?format=api",
"text_counter": 56,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Halake",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13184,
"legal_name": "Abshiro Soka Halake",
"slug": "abshiro-soka-halake"
},
"content": "Simjui binafsi lakini ningependa kuwapa pole kwa sababu huu ni wakati mgumu sana kwa familia ya mwendazake. Hata hivyo, sisi kama Wabunge ni familia yake pia. Sitaki kusema sana ila tu kuwaombea Mungu awape subra wakati huu mgumu wa buria. Vile vile awape wananchi na Wabunge wa Uganda subra katika mambo yao. Sisi kama Waislamu tunashukuru kwa kila kitu. Hata katika kifo, tunampa Mungu shukrani kumuonyesha kwamba hata kama sisi binadamu tunajua mengi, kuna mengi ambayo hatujui na Mungu ndiye hutupa maisha na tunarudi kwake tukishamaliza safari yetu hapa duniani. Nawapa pole na Mungu amlaze pema peponi alipowalaza wale wema mbele yake."
}