GET /api/v0.1/hansard/entries/1160792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160792/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ili niweze kutoa rambirambi zangu kwa familia ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda na Wabunge wa Uganda ambao najua wamechaguwa Spika mwingine. Wamempoteza mtu shupavu. Kazi ya Spika ni kama ya refarii ambaye anaketi pale kutupa sisi nafasi ili tuweze kutetea wananchi ambao walituleta hapa. Kwa kweli, ni jambo la kuhuzunisha kumpoteza kiongozi kama huyo. Ningependa kuwajulisha watu wa Uganda kwamba sisi kama Wakenya, katika uwiano wetu wa jumuiya ya kimataifa, tunawapa pole. Tunawaombea ili Mola awape nguvu ya kuendelea na maisha. Tunajua kuwa Maisha yetu duniani ni siku chache sana. Kifo kinatukumbusha kuwa wakati tuko hai lazima tufanye ile kazi iliyotuleta duniani ili tuweze kuwasaidia wananchi ambao wanatuamini kuwafanyia kazi nzuri. Asante Bw. Spika wa Muda."
}