GET /api/v0.1/hansard/entries/1160799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160799/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "zinataja kwamba shughuli zote za Seneti zitaendeshwa kwa Kiswahili, Kiingereza au katika Lugha Ishara ya Kenya. Waheshimiwa Maseneta, uzingatiaji wa masharti yaliyotajwa hapo juu ya Kanuni za Kudumu umekuwa na changamoto hasa wakati ambapo hotuba ya Seneta ipo katika Kiswahili na angependa kunukuu sehemu fulani ya Kanuni za Kudumu. Maoni pia yametolewa kuhusu umuhimu wa kutafsiri Kanuni za Kudumu za Seneti katika Kiswahili ili kuweza kufungua shughuli za Seneti kwa sehemu kubwa ya umma wa Kenya, ambao huitumia lugha hii katika shughuli zao za kila siku. Kamati ya Uratibu na Kanuni iliamua kwamba Kanuni za Kudumu za Seneti zitafsiriwe kwa Kiswahili. Katibu wa Seneti aliunda Jopokazi la Tafsiri ya Kanuni za Kudumu za Seneti lililojumuisha maafisa wa Seneti. Katika kufanya shughuli hii, Jopokazi lilitafuta usaidizi wa wasomi watajika wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Moi. Kwa kuongezea, Jopokazi lilifaidi pakubwa kutokana na ujuzi wa Maseneta wawili, Sen. (Dkt.) Agnes Zani, CBS, na Sen. (Dkt.) Isaac Mwaura, CBS. Jopokazi hili lilitekeleza shughuli hii na kufanya mikutano kadha ya uidhinishaji na kuwasilisha ripoti yake kwa Bodi ya Usimamizi ya Seneti. Baadaye, ripoti hiyo na nakala iliyotafsiriwa ya Kiswahili ya Kanuni za Kudumu ziliwasilishwa kwa Kamati ya Uratibu na Kanuni. Katika mkutano wake uliofanyika tarehe 8 Julai, 2021, Kamati ya Uratibu na Kanuni ilizingatia na kuidhinisha Kanuni za Kudumu za Seneti na nakala ya uwililugha. Ninafuraha kuijulisha Seneti kwamba Kanuni za Kudumu za Seneti na Kanuni za Kudumu za Uwililugha sasa zimechapishwa na zitasambazwa kwa Maseneta wote. Kwa niaba ya Seneti, ningependa kumshukuru Katibu wa Seneti na Jopokazi la kutafsiri Kanuni za Kudumu za Seneti likiongozwa na Bw. Lawrence Amolo kwa kutafsiri na uchapishaji wa Kanuni hizi. Pili, shukrani zetu kama Seneti zinawaendea Makamu Wakuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Moi kwa kuwaruhusu wasomi watajika wa Kiswahili kusaidia katika tafsiri. Wasomi hawa ni: (1) Prof. Iribe Mwangi - Chuo Kikuu cha Nairobi"
}