GET /api/v0.1/hansard/entries/1160805/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160805,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160805/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "- Mwanachama 8. Sen. (Dkt.) Agnes Zani, CBS, - Mwanachama 9. Sen. (Mhasibu) Farhiya Haji, - Mwanachama Waheshimiwa Maseneta, shughuli hii imechukua muda mrefu lakini kama mnavyojua, wahenga walisema, kawia ufike. Kwa sasa hivi, ndio mwanzo mkoko unaalika maua. Kuzinduliwa kwa Kanuni hizi za Kudumu katika lugha ya Kiswahili ni jambo muhimu sana la kujivunia na tajika katika historia yetu kama nchi na kama Bunge la Seneti. Ningependa kuwasihi nyinyi nyote mfanye jitihada ili mfanikishe matumizi ya Kiswahili katika shughuli za Seneti. Hii itatuwezesha kuwasiliana barabara na wadau wetu ambao tunawakilisha ikizingatiwa kuwa mke ni nguo, mgomba kupalilia. Ninawashukuru. Asante sana kwa kunisikiza. Sen. Madzayo, kabla hujasema lolote ningependa kuwajulisha ya kwamba nakala ya Kanuni za Kudumu pamoja na nakala ya uwililugha zitapatikana katika hili jumba letu kule the journals room."
}