GET /api/v0.1/hansard/entries/1160817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160817,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160817/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, kwa kumalizia, vile umesema mkoko ndio sasa unaanika maua, ni kumaanisha ya kwamba hakuna mwisho wa Kiswahili. Ikiwa mkoko umeanza kuanika maua sasa, ikiwa hizi kanuni za kudumu zitapatikana kuna kwengine kumekosewa na kwengine kutataka kurekebishwa, litakuwa jambo zuri sana. Nina hakika ya kwamba sio sisi tu bunge la Seneti limefika mwisho lakini hatimaye wale watakaokuja wakiwa wanataka kujifundisha ama kuongea Kiswahili ama kuongea kwa lugha ile ya Ishara am lugha ya Kizungu, basi watafaidika na hizi nakala ambazo tuko nazo."
}