GET /api/v0.1/hansard/entries/1160840/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1160840,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1160840/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Sasa hiyo ni nini tena? Ningependa kuona ya kwamba, Kama vile Quran pengine imeandikwa kwa lugha nyingi au pengine Biblia imeandikiwa kwa lugha zote, ni vizuri pia watu wale ambao wako nyumbani ambao wangependa kuwa viongozi waweze pia kujua hizi Kanuni Za Kudumu za Seneti zinasema nini. Hayo ni mambo ambayo watu wengi hawajui. Ninawashukuru sana nyinyi ambao mliketi, mkaweka akili zenu zote hapo na kuweza kutafsiri kutoka lugha ya Kizungu hadi lugha ya Kiswahili. Siku moja tutatafsiri kwa lugha ya Kikamba, Kipokot, Kigiriama na Kiborana, lakini Kigiriama ni kama Kiswahili tu. Haya mambo ambayo najaribu sana kutafuta matamshi ambayo nitatumia kuweza kusisitiza ni mambo ambayo yatatusaidia kama Wakenya. Yatatusaidia kwa sababu kama mimi sasa niko hapa ninaanza kujifunza Kiswahili. Mimi sikuwa ninajua Kiswahili. Nimeishi Marekani miaka 20 na ninajaribu pole pole. Zikiwekwa kwa Kimaasai zitatusaidia tuendelee. Wale watoto ama wamama ambao hawakupata nafasi, tunaweza kuwaambia hizi Standing Orders zetu zinasema hivi na vile. Kama vile Katiba imetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili, naomba ya kwamba itafika wakati ambapo itawekwa katika lugha zote tulizonazo hapa Kenya. Nitajaribu sana kuzungumza Kiswahili. Huenda nisiweze kwa sababu leo kuna Hoja muhimu sana kuhusu fedha ambazo zinatakiwa kutumwa katika kaunti. Hiyo utaniruhusu tu niongee Kizungu kwa sababu sitajua ya kusema. Asante Bw. Spika wa Muda."
}