GET /api/v0.1/hansard/entries/1161055/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1161055,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161055/?format=api",
"text_counter": 321,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ili tuweze kusonga mbele kwa Hoja ambayo tuko nayo leo, nikiangalia katika Kanuni za Kudumu ile ambayo mwenzangu Sen. Sakaja amezungumzia, inasema ya kwamba- “iwapo Seneta ana sababu ya kumshawishi Spika kwamba Seneta anayechangia hawezi kuthibitisha madai yake papo hapo, Spika atamhitaji Seneta anayechangia kuthibitisha madai yake, isiwe baada ya kikao kinachofuata.” Bw. Spika wa Muda, ningeomba hivi, kwa sababu tunataka tuendelee kuzungumzia maneno ambayo yametuleta hapa leo, kama mwenzangu, Sen. Sakaja, hajaridhishwa na mambo ambayo Seneta kutoka Kaunti ya Nyamira ameyataja hapa, ampe muda ule ambao umepewa katika Kanuni za Kudumu ili tuweze kuendelea."
}