GET /api/v0.1/hansard/entries/1161198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1161198,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161198/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kanuni 48(1) ya Kanuni Za Kudumu za Seneti kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Barabara na Uchukuzi kuhusu ujenzi wa Mahakama mpya katika Kaunti ya Mombasa. Bi. Naibu Spika, katika Kauli hiyo, Kamati inapaswa kuangazia yafuatayo: (1) Kueleza kilichosababisha jumba hilo la mahakama kuwa na nyufa hata kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Tume ya Mahakama nchini. (2)Kueleza aliyepewa kandarasi ya ujenzi huo na sababu za kutokuwa na usimamizi wa kisawasawa wa kandarasi hiyo. Kueleza japo jumba hilo limeidhinishwa rasmi na kaunti ilhali usalama wa watumiaji wa jumba hilo haujahakikishiwa. (3)Kutaja hatua zitakazochukuliwa na Serikali ya Kitaifa kuhakikisha kuwa jumba hilo ni salama kwa matumizi ya maelfu ya wananchi ambao, wengi wao hutegemea jumba hilo kutafuta haki wanapodhulimiwa. Bi. Naibu Spika, jumba hili lina historia kidogo, kwa sababu ile ardhi wakati fulani ilikuwa imenyakuliwa na mwekezaji wa kibinafsi. Mimi pamoja na mawakili wenzangu tulienda mahakamani tukahakikisha kwamba ardhi hiyo imerejea kuwa ya mahakama. Itakuwa ni kinyume na matarijio yetu kwamba kutajengwa mahakama pale ambayo tayari imeweza kutoa nyufa kabla jumba hilo halijaweza kukaliwa. Bi. Naibu Spika, ikikumbukwa kwamba mahakama ya kwanza Mombasa ilijengwa mwaka wa 1903, na mpaka leo mahakama hiyo iko na inatumika na vilevile ni thabiti kuliko lile imejengwa hivi sasa. Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii."
}