GET /api/v0.1/hansard/entries/1161284/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1161284,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161284/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi. Uchaguzi ni gharama kubwa sio kwa serikali pekee yake lakini pia kwa wagombea tofauti ambao wanagombea viti tofauti katika uchaguzi huo. Kuna haja ya kudhibiti matumizi wakati huu wa uchaguzi kwa sababu kuna wengine ambao wako tayari kununua uchaguzi ili sauti ya wale ambao wana haki au wale wanyonge isiweze kusikizwa. Kwa hivyo Mswada huu umekuja wakati muafaka, wakati tunajitayarisha kuenda katika uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mwezi wa nane mwaka huu. Itasaidia pakubwa sheria hii ikipitishwa ili kuweka wazi na kudibiti matumizi wakati huu wa uchaguzi. Tumeona kwamba sheria iliyoko sasa ina mapungufu fulani kwa sababu ni vigumu kwa Auditor-General au Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kuweza kuwakagua wanasiasa wote ambao wanagombania viti katika uchaguzi. Tumeelezwa hapa kwamba chama kimoja tayari kina wagombea 5,000 wakati Mkaguzi Mkuu inamchukuwa zaidi ya mwaka kuweza kuwakilisha ripoti za kaunti 47 na mabunge ya kaunti 47 ambayo yako katika inchi yetu. Kwa hivyo, watu 5,000 au zaidi ya 10,000 ambao watagombania viti tofauti, itakuwa ni shida sana kwao kumpata Mkaguzi Mkuu wa serikali ili akague na kuona ya kwamba hesabu zao ziko sawa sawa. Kwa hivyo, kuna haja ya kudhibiti sheria hii ili tuone kwamba watu hawapotezi nafasi zao au kutumia matumizi zaidi ya yale ambayo sheria inasema. Tumeona hapo nyuma ya kwamba hivi sasa tayari wagombea tofauti wameweza kutumia fedha kinyume ya sheria. Utaona kwamba wengine walianza kampeni mwezi ya sita mwaka wa jana na pia utaona mabango sehemu tofauti; wengine nao walianza miaka tano iliyopita wakisema kumi yako, kumi yangu. Kwa hivyo, tayari sheria imekiukwa lakini nafikiri kuwepo kwa sheria hii itasaidia pakubwa kuweza kuweka laini mambo ya fedha ya kila mgombea. Kulingana na sheria hii, haitakikani Mkaguzi Mkuu akuje kukuambia utoe hesabu zako. Inavyopendekezwa katika sheria ni kwamba kila chama kitaweza kupeleka hesabu zake na hiyo itasaidia pakubwa kupunguza ile kazi ambayo Mkaguzi Mkuu wa serikali angeweza kufanya."
}