GET /api/v0.1/hansard/entries/1161461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1161461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161461/?format=api",
"text_counter": 57,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuleta Hoja ya nidhamu. Mwaka jana, tulileta Taarifa hapa kuhusiana na kutolipwa mishahara kwa wafanyikazi wa Shirika la Posta la Kenya . Taarifa hiyo ilipelekwa kwa Kamati ya Habari, Teknolojia na Mawasiliano. Baadaye, walileta taarifa hapa iliyosema mishahara imelipwa. Hata hivyo, jambo hili limekuwa likirudiwa kila mara. Ninapozungumza hapa leo, miezi mitatu imepita sasa tangu wafanyikazi wote wa Shirika la Posta la Kenya hawajalipwa mishahara. Ni jambo la aibu tena la kusikitisha, kwamba Shirika kama hili ambalo lilikuwa na nguvu na uwezo hapo nyuma, sasa linawadhalilisha na kuwatesa wafanyikazi wake. Sasa hawawezi kumudu maisha.. Bi. Spika wa Muda, ninaomba Kamati hii irudie swala hili. Iwapo swala hili limekuwa shida kwa Kamati ya Habari, Teknolojia na Mawasiliano, basi lipelekwe kwa Kamati ya Kazi na Ustawi wa Jamii ili waliingilie kwa makini zaidi. Kamati ya Kazi na Ustawi wa Jamii ina uzoefu wa mambo ya mishahara na haki za wafanyajikazi. Bi. Spika wa Muda, ilikuwa ni wakati wa homa ya korona ambapo walisema kuwa hawakuweza kufanya kazi vizuri. Homa ya korona imepungua hadi sasa haizungumziwi. Watu wanazungumzia maswala ya Urusi na Ukraine. Kwa hivyo, hili swala lazima tuli---"
}