GET /api/v0.1/hansard/entries/1161530/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1161530,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161530/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "maeneo yao. Vilevile, miradi wanayoifanya inaanza kukamilika na hivyo kuhitaji pesa nyingi kuweza kutekelezwa kila mwaka. Kwa hivyo, ongezeko la pesa italeta afueni sana kwa kaunti zetu kwa sababu pesa hizo zitasaidia pakubwa katika kurahisisha huduma. Kuna mambo matano ningependa kugusia katika swala hili. La kwanza, kuna pesa za Managed Equipment Services (MES). Hapo nyuma, Kamati yetu ya Seneti iliyochunguza mradi huu ilipata kulikuwa na utepetevu mwingi katika kupeleka hivi vifaa kwenye kaunti zetu. Mpaka sasa, kuna kaunti zingine ambazo hazijaweza kutumia vifaa vile. Uchunguzi nilioufanya ni kwamba ongezeko la Kshs7 bilioni utasaidia kufunga pengo lililoko sababu kandarasi nyingi zinakamilika mwaka huu. Hakuna mipango yeyote iliyofanywa kuweza kuzifungua tena upya ili ule mradi huweze kuendelea. Kaunti zimelipa pesa nyingi na hatima ya vifaa vile haijajulikana. Hatujui kwa mfano kama watakuja wachukue vifaa vyao maana ilikuwa ni kukodisha. Walikua wamekodisha kisheria na kama umekodisha chombo chochote kisheria, ni lazima baada ya yule muhula kuisha ukirejeshe kwa mwenyewe. Hatujui hatima ya vile vifaa vilivyochukuliwa wakati ule. Je, vitarejeshwa kwa zile kaunti ama mwenye kuzikodisha atazichukua na kuziuza sehemu zingine? Kuna maswala ya vile vyombo ambavyo havikuweza kutumika. Kwa mfano, tulipozunguka na Kamati ya Covid-19, tulifika hospitali nyingine tukaona vifaa vinavyohitajika kutumika kama dialysis machine lakini hospitali haikuwa na maji ya kutosha ili kutumia vile vifaa vya dialysis ambavyo vinahitaji maji yaliyosafishwa kikamilifu. Sehemu zingine zilikua na mashine za X-ray lakini hazikuweza kutumika kwa sababu hospitali au zahanati hazikuwa na umeme. Ina maana kwamba, kaunti imelipia pesa kwa muda wa miaka mitano au kumi lakini vifaa havijaweza kutumika kabisa katika sehemu zile. Zingine zilikua zinaharibika kidogo lakini hakukuwa na wataalamu ambao wangesaidia kurekebisha kwa haraka ili wanainchi waendelee kupata huduma. Jambo lingine ni kwamba tuliona hapo nyuma kwamba Baraza la Magavana walipinga kuzinduliwa upya ama kuongezwa kwa kandarasi hii. Kwa hakika walikua na sababu zao. Swala la hivi vifaa ni kaunti zinanzoangalia mbele kama Mombasa, zimetumia vifaa vile na kupata pesa nyingi ambazo zimefidia zile wanazokatwa kulipia vile vifaa. Kaunti zinazoangalia mbele zimetumia vifaa kikamilifu na kupata pesa nyingi kwa sababu zimesaidia kuleta huduma karibu na mwananchi. Ukiangalia kwa sasa, huduma za X-ray hazipatikani sehemu zingine kabisa. Inambidi mgonjwa kwenda na kurudi hospitalini akisubiri huduma hii. Kaunti zinazoangalia mbele zimeweza kutumia vifaa hivi vizuri sana na kupata pesa nyingi kutokana na matumizi yao. Kaunti ambazo ziko katika fikra za nyuma zimepata hasara kwa sababu pesa zimeenda, ilhali vifaa havijatumika kisawasawa. Iwapo tutakubaliana kwamba pesa hizi ziwekwe katika hii sheria, lazima tuwe na uhakika vile zitatumika na kuwe na mikataba maalum baina ya serikali za kaunti ili zisiletewe vifaa zisivyohitaji. Kaunti zingine zimepelekewa vifaa zisisohitaji. Ina maana kuwa pesa imetumika kwa njia isiyokuwa sawa."
}