GET /api/v0.1/hansard/entries/1161532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1161532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161532/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kaunti zingine bado zinasubiri Serikali kuu ilete fedha ilhali tumeona kwamba Serikali kuu pia imebanwa katika matumizi yake. Utapata kwamba mara nyingi inachelewa kupeleka pesa kwenye kaunti na hivyo kuna kuwa na misukosuko. Wafanyi kazi hawajui watapata mishahara yao lini na huduma zinadorora katika kaunti zetu. Njia ya kutatua swala hili ni kaunti zidhibiti njia zao za kuokota kodi katika maeneo yao. Sehemu nyingi zinakusanya kodi kizamani. Utapata afisa wa kaunti anazunguka barabarani na kitabu cha risiti akikusanya fedha za kaunti. Hii imepitwa na wakati kwa sababu haijulikana kama wanarudisha pesa hizi kisawasawa. Wengine wanachapisha vitabu vyao wanapozunguka kukusanya kodi. Hivyo basi mapato kamili ya kaunti zile hayajulikani. Ni lazima kaunti zidhibiti mapato yake kwa sabau hiyo ndio njia pekee itakayofanya wajiokoe kutokana na hili lindi la kuomba kila siku kutoka kwa Serikali kuu. Kwa hivyo tupitisha sheria hii na kutoa muongozo wa lini pesa zitalipwa. Mara kwa mara, utapata wizara ya fedha imechelewesha malipo kwa kaunti na kusababisha huduma kudorora. Bi. Spika wa Muda, jambo la tatu ni swala la uangalizi wa kaunti hizi. Kama alivyotangulia kusema Sen. Cherargei, Maseneta hawana jukumu lolote baada ya kupitisha sheria hii na pesa kuenda katika kaunti. Hawana jukumu lolote mpaka Mhasibu Mkuu alete ripoti katika Bunge hili kusema kwamba pesa hizi hazikutumika vizuri katika sehemu hii. Ijapokuwa sisi tunatoka katika kaunti zile, hatuna utaalamu wa kutosha kuweza kuangalia tukasema katika ripoti zetu kwamba hii barabara imegharimu milioni mia moja au milioni ishirini kutokana na vile imetengenezwa. Swala la pesa za evaluation andmonitoring kwa maseneta ni swala muhimu kabisa kwa sababu hiyo ndio itasaidia pakubwa kuweza kujua kama pesa zile zimetumika kikamilifu au la. Tunaona kwamba Maseneta wengine wana kaunti kubwa ambazo huwezi kuzitembea peke yao bila ya usaidizi wa feda zaidi kutokana na hizi pesa ambazo tunazoitishwa za evaluation and monitoring. Kwa hivyo, hili ni swala ambalo lazima kama tunataka ugatuzi ufaulu, lazima iwe kuna nafasi ya Maseneta kupata fursa ya kutembelea miradi pamoja na maafisa wa kitaalamu na kuhakikisha kwamba kweli fedha zinatumika kisawasawa katika miradi. La sivyo itakuwa tunasubiri ripoti za postmortem baada ya mambo ishafanyika ndio tunaletewa ripoti hapa miaka minne au mitano baadaye kuja kuangalia kama pesa ilitumika kisawasawa au la. Sisi Maseneta tunatumika kama wale wanaofanya uchunguzi wa postmorterm . Yani mambo yameshafanyika miaka minne mitano ndio tunarudi kuitwa sisi kama Maseneta kuwachunguza. Hiyo haitasaidia ugatuzi kwa sababu ugatuzi inataka huduma ziweze kutolewa mwaka ule kama hazikutolewa tujuwe kwa nini hazikutolewa mwaka ule. Kusubiri miaka mitatu au minne baadaye haisaidii. Tumeona kuwa ipo haja ya kuangalia tena zile huduma ambazo zinatolewa na kaunti zetu kwa mfano, huduma za afya. Ijapokuwa ni muhimu na ziligatuliwa lakini kuna wengi wanaosema kuwa huduma hii inafaa irejeshwe kwa serikali kuu kwa sababu wananchi bado wanapata shida katika sehemu nyingi. Migomo haimaliziki na utapata kwamba wanaohujumiwa zaidi ni wafanyikazi wa afya ambao wanaodumia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao."
}