GET /api/v0.1/hansard/entries/1161534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1161534,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1161534/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Mheshimiwa Spika, tunaona migomo kila mara. Kwa mfano, Kaunti ya Mombasa imekuwa na migomo mara kwa mara ya madaktari kwa sababu ya kucheleweshwa kulipwa kwa mshahara na malumbukizi ya madeni pamoja na zile mikato ya kisheria kama National Hospital Insurance Fund (NHIF), National Social Security Fund (NSSF) na mengineo. Hata kodi ya income tax inacheleweshwa kulipwa katika Kenya Revenue Authority (KRA) na inasababisha wananchi wengi kupata shida ya kuweza kupata mikopo au kuweza kulipwa mikipo yao ambayo wamechukuwa katika bengi na taasisi nyingine za kibinafsi. Ipo haja ya kuweza kuangalia tena hii mfumo wa ugatuzi kuhusiana na vile ambavyo tutaweza kuviboresha kaunti zetu kwa sababu mifumo ambao uko sasa wa maendeleo na vile wa usimamizi unatoa fursa kubwa kuhakikisha kwamba mambo mengi yanafanyika katika kaunti zetu bila ya kuwa na uangalizi ya kutosha. Juzi nilibahatika na kamati yangu kuweza kuangalia kanuni ambazo zililetwa katika kamati yetu ya Mamlaka Kasimishwa kuhusiana na vile ambavyo mdhibiti Bajeti ataweza kuhakikisha kwamba kuna stakabadhi za kisawasawa ili aweze kutoa pes a zile. Ijapokuwa tuliona zile kanuni zimeletwa kwa njia nzuri, tuliona kwamba upo unyonge mkubwa katika ofisi ya Mdhibiti Bajeti. Kwanza, ofisi ile haipati fedha za kutosha. Vile, kazi ambayo wanatakakikana kufanya ni kazi kubwa kabisa kwa sababu kuangalia kaunti arubaini na saba, kuangalia pia na serikali kuu ambayo ina wizara zaidi ya ishirini zote zina karibu kaunti na taasisi karibu sitini na saba. Ikiwa hawakupata fedha za kutosha inamaanisha kwamba matumizi ya fedha katika kaunti hizi yatakuwa bila uangalizi wa kisawasawa. Kwa hivyo, ipo haja ya kutilia nguvu ugatuzi na uwazi katika ugawaji wa fedha katika upelekaji wa pesa katika serikali. Hii ofisi ya Mdhibiti Bajeti lazima itiliwe nguvu kwa sababu ni kitengo muhimu katika maswala ya fedha na kuleta uwazi katika usimamizi wa fedha katika serikali yetu. Naunga mkono Mswada huu kwa kuwa ni wa mwisho kabla ya kwenda katika uchaguzi. Ningependa kuipongeza Serikali kwa kuongeza fedha hizo. Wale waliokuwa wakisema kwamba mkurupuko wa mabeo umeongezeka, mambo haya ni mbegu ambazo zilipandwa mwaka elfu mbili kumi na tatu mpaka kumi na saba na sasa ndizo zinaonesha matunda yake kwa sababu ya Handshake au uelewano uliofanyika baina ya Rais Kenyatta na Mhe. Raila Amolo Odinga. Umeleta utulivu katika uchumi na usalama katika nchi yetu na vile kutoa nafasi ya maendeleo kufanyika. Nairobi Expressway iko karibu kuwa tayari. Kule Mombasa, barabara yetu ya Makupa Courseway iko tayari. Daraja pia nafikiri iko tayari. Katika muda wa miezi mitatu au minne tutakuwa na daraja mpya katika Makupa Courseway badala ya Makupa Courseway, tutakuwa daraja la Makupa. Katika sehemu nyingi tumeona barabara zikijengwa na maendeleo yameweza kusongea katika kaunti hizi. Kwa hivyo ule uelewano baina ya Rais Kenyatta pamoja na Mhe. Raila Amolo Odinga umesaidia pakubwa kuleta utulivu ule kwa sababu yale yote ambayo serikali ya Jubilee iliahidi katika muhula wake wa kwanza kama stadium, laptop, mabwawa ambayo yalikusudiwa kujengwa kama Arror na Kimwaror hatukuyaona ijapokuwa pesa zililipwa kufadhili miradi hiyo. maendeleo yamekuja sasa. Hii budget ya mwaka huu kuhusiana na"
}