GET /api/v0.1/hansard/entries/1163063/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163063,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163063/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kujiunga na hio Kauli ya Nidhamu ambayo imeletwa na ndugu yetu Sen. Omogeni. Jambo la kwanza, nilikua katika hio safari ya kuenda ulaya na Sen. Omogeni. Utaona ya kwamba kutoka nchini kulikumbwa na maswali kwa kuwa hakukuwa na ruhusa ya kutoka nchini kwa kuwa kuna barua kutoka Serikali. Niliwauliza wanionyeshe barua hiyo ambayo inazuia mmbunge kufanya kazi yake. Tukitoka hapa, sisi huwa na idhini ya Bunge hili. Ikiwa barua ile imeandikwa na wewe mwenyewe kama Spika na umeandika kuwa huyu Seneta ameenda safari ya kikazi lakini tunaona kama barua hiyo imepuuzwa na kuna nyingine imekuja na kuzimisha uwezo ya Spika wa bunge hili. Tukitoka hapa hatutoki kama wakora. Tunatoka kama viongozi ambao wanafanya kazi ya Serikali na kazi ya bunge hili ambavyo inatakikana kufanywa. Kurudi kwangu ilikuwa juzi na mimi pia nilizuiliwa katika uwanja wa ndege. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba kiongozi anatoka safarini na kuambiwa asonge kando kwa sababu mambo yake yanaangaliwa. Nilikuwa hakimu katika mahakama Kuu ya Kenya, sijawai fanya kosa wala kupelekwa katika kituo cha polisi hata siku moja. Sijawahi kufanya kitu ambacho kinaweza kunifanya mimi kuchunguzwa katika mambo ya ufisadi au jambo lolote lile. Nilikua na tashwishi sana."
}