GET /api/v0.1/hansard/entries/1163481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163481,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163481/?format=api",
    "text_counter": 495,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa hii fursa, ili kuchangia Hoja hii ya Sen. Nyamunga kuhusu suala la kusaidia wazee ambao wamefikisha miaka 70 na wanahitaji misaada. Kwanza ningependa kushukuru Serikali yetu ya Kitaifa kwa kuanza mpango mzuri wa Inua Jamii. Huu mpango umesaidia hawa wazee wetu ambao ni baba, mama na ndugu zetu lakini kwa vile wameishi maisha mazuri ya kumcha Mungu wameishi miaka mingi na wamefika mahali ambapo tunapaswa kuwasaidia. Mpango wa Inua Jamii ni mpango ambao umesaidia wazee wetu kuishi maisha mazuri. Lakini huu mpango umekumbwa na changamoto nyingi kwa mfano ile pesa inayopeanwa ya Kshs2,000 haitoshi. Nikiwa mwenye kiti mdogo wa Kamati ya Labour na Social Welfare, tumejaribu kusukuma na kushinikiza Serikali iongeze hii pesa kwa sababu hao wazee wanaopewa Kshs2,000 kwa Bajeti, kulingana na mfumko wa bei za vitu haitoshi. Pia pesa hizi haziji kwa muda unaofaa, zinachelewa sana. Zinakuja baada ya miezi mitatu ama minne. Zikichelewa kwa muda wa miezi minne, hao wazee wanatumia nini? Wanapata shida nyingi sana. Ni vizuri pesa hizi zije kwa wakati unaofaa. Changamoto nyingine ambayo imekumba huu mradi wa serikali wa Inua Jamii ni kwamba Serikali haiandikishi watu wapya. Wale ambao wako wamefikia miaka 70 tayari wanapata pesa. Hao wengine ambao wanafikiwa wapya hawaandikishwi. Tumejaribu kuuliza Serikali kwa nini hawaandikishi hawa wazee wetu, na inasema ni shida ya kibajeti. Lakini ingekuwa ni vyema kuwasajili hawa wazee wote ambao wamefikisha umri wa 70 na tuwe na Bajeti ya kutosha ili wafaidike na mpango huu wa Inua Jamii. Kuna wazee wengine ambao walikuwa wanapata hizi pesa lakini kwa sasa hivi wameaga dunia na Serikali hajawasajili wapya ili waweze wakipata hizo pesa. Kwa hivyo, ningeomba pia Serikali---"
}