GET /api/v0.1/hansard/entries/1163506/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163506,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163506/?format=api",
    "text_counter": 19,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Ardhilhali hii. Mambo ya walimu wa chekechea imekuwa donda sugu kwa sababu kulipwa mishahara kwao imeakuwa kama jambo ambalo halijawekwa katika daftari zetu. Inakuwa jambo ambalo linafanywa kiholela. Ukitembea sehemu nyingi humu nchini, walimu hawa wa shule za chekechea hawashugulikiwi kwa lolote na hawalipwi mshahara yao kwa nyakati zinazofaa. Isitoshe, wanapokea hela kidogo sana ambazo haziwezi kuwatosha kujikimu kimaisha ilhali tunawategemea zaidi kwa sababu ya wale wanafunzi wa chekechea. Walimu wa chekechea wamepewa jukumu nyeti katika maisha ya watoto wetu lakini Serikali yetu hailipi chochote. Walimu hao wamekuwa wakisumbuka na kuhangaika. Kwa mfano, katika Kaunti ya Laikipia, walimu wa chekechea wanaweza kukaa zaidi ya miezi minne kabla hawajapokea mishahara yao ilhali wanafanya kazi yao kwa ushujaa na weledi. Naomba kaunti zetu zitenge pesa na ziamuru kuwa walimu wote wa chekechea walipwe kiwango fulani. Isiwe wanalipwa kiholela. Walimu wa chekechea wanalipwa mishahara tofauti katika kaunti zetu. Katika Kaunti ya Laikipia, walimu hao wanalipwa Ksh10,000 na fedha hizo zinatofautiana katika kila kaunti. Nakubaliana na walaminishi walioleta Ardhilhali hii hapa Seneti. Mambo ya walimu wa chekechea lazima yaangaliwe kwa undani na maswala yao kuangaziwa. Walimu wa chekechekea hawana bima ya afya. Hawawezi kuhudumiwa na serikali. Baraza la Magavana linafaa kuhusika ili wahudumiwe vizuri ndiposa malipo yote ya walimu wa chekechea katika kaunti zote kama Isiolo, Lamu na pia Laikipia yawe sawa kwa sababu wale ndio wanaanza kufunza watoto kusoma. Tunafaa kuwapa kipaumbele"
}