GET /api/v0.1/hansard/entries/1163632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163632,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163632/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi. Naunga mkono Taarifa ya Sen. Khaniri. Hakika, sisi kukuza mali yetu kama Wakenya na pia talanta zetu ndani ya Kenya ni jambo muhimu kuliko kuleta vitu kutoka nje. Biashara nyingi zimekuwa za watu wa kutoka nje, hasa Wachina nchini. Kama vile Senata mwenzangu alivyosema, sisi pia Wakenya tumeingia katika ubumbuwazi wa akili ya kwamba vitu vya Kenya ni vitu ambavyo havifai. Ndio kwa sababu wengine wanasema hawawezi kuvaa nguo ambazo zinatoka Kenya, mpaka wavae nguo za nje. Ni jambo la busara kukuza talanta na biashara zetu ndani ya Kenya. Hii njia ambao itanua maisha ya Wakenya, hasa wale ambao wanafanya biashara ndogo ndogo. Tunaweza kukuza na kuuza mali ya Kenya ndani ya Kenya. Hii itakuwa ni desturi kubwa na ya manufaa makubwa kuliko sisi kuzingatia kwamba vitu vya Kenya na talanta za Kenya na biashara ya Kenya ni vitu ambavyo ni duni kuliko za kutoka nje. Hii ndio sababu Wachina wameleta biashara kubwa kubwa na kuzishikilia. Hivi sasa wanataka kuuza hata maandazi ndani ya Kenya. Kwa hivyo, mimi ninaunga mkono Taarifa ambayo imetolewa na Sen. Khaniri."
}