GET /api/v0.1/hansard/entries/1163643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163643/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi. Naunga mkono Taarifa ya Sen. Kasanga. Kwa kweli, uraibu wa vitu vya kisasa, hasa na vijana, umekuwa changamoto katika jamii. Kuna uraibu wa aina mbali mbali. Mara nyingi watu huwa na uraibu wa pombe na mambo mengine kadha wa kadha. Jamii ya kesho, ambayo ni vijana wa leo, ina kasumba ya ulevi na uraibu wa vitu tofauti tofauti. Kwa hakika, vijana hao ni wazembe kwa sababu ya ulevi na uraibu wa vitu vingine. Iwapo jambo hili halitaangaliwa kwa kina ili kukomesha vijana kutokana na uraibu wa vitu tofauti tofauti, basi siku zijazo tutakuwa na jamii ambayo haitafanya kazi na utendakazi utakuwa wa chini sana. Kenya itajaa watu wazembe; watu ambao hawatafanya kazi ili kuzalisha mazao mashambani. Bw. Spika wa Muda, ifahamike kuwa wafugaji pia wameanza kuwa na uzembe. Ufugaji ambayo wewe na mimi tunafanya hauwezi kufanya na vijana wa sasa kwa sababu ya ulevi na uraibu wa vitu tofauti tofauti. Taarifa hii inafaa ishughulikiwe na Kamati ili ijadiliwe kwa kina. Wanafaa kuangalia nini kinawezafanywa ili kukomesha uraibu ambao vijana wameingilia. Ukienda katika Mwambao wa Pwani, utakuta watu wameingia katika biashara mbaya ya vitu vya kutoka nje. Vile vile, kuna watu ambao wamejitayarisha kutokana na kuuza mihadarati kwa vijana wetu. Kwa hivyo, kuwafanya kuwa wazembe kwa sababu ya ulevi na uraibu wa dawa za kulevya. Kwa kiingereza, inajulikana kama substanceabuse . Endapo hali hii itaendelea, tutakuwa na jamii ya watu wazembe kwa sababu ya ulevi. Hatutakuwa na utendakazi mzuri. Watu hawatafanya kazi mashambani na hatutakuwa na ufugaji na biashara. Watu watakuwa wakikaa chini ya miti kungojea mambo yatendeke kimiujiza. Hiyo haitawezekana isipokuwa kuwa na watendakazi humu nchini na duniani. Naunga mkono."
}