GET /api/v0.1/hansard/entries/1163654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163654,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163654/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Wakenya wengi wako gizani na wanataka kujua mwelekeo wa ujenzi wa hii Expressway. Hii Expressway ambayo imejengwa kutoka huko uwanja wa ndege wa JKIA na kupita hapa nyuma ya Bunge ndio barabara ninayotumia nikitoka nyumbani kwangu. Wakenya wengi wanauliza kuhusu ujenzi wa hii Expressway. Kwa lugha ya Kiswahili express inamaanisha kupita moja kwa moja bila kusimama. Najua Bw. Spika wa Muda ni Mswahili na anaweza kufafanua vizuri haya mambo ya Expressway. Hii Expressway ilikuwa ikamilike Desemba mwaka jana na itumike lakini mpaka leo tunaona bado watu wanaendelea kuijenga. Nadhani huu mradi ni wa Wachina. Tungetaka kujua kutoka kwa Kamati tekelezi; pesa iliongezwa kwa sababu gani? Pili,"
}