GET /api/v0.1/hansard/entries/1163656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163656,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163656/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "tulielezwa kuwa Desemba kazi hii itakuwa imeisha na bado haijaisha. Inaonekana hata hii Desemba ijayo hii kazi haitakuwa imekamilika. Tulitaka matunda ya Rais Uhuru, kuja kutuonyesha magari ikipita juu. Ile kazi inayoendelea sio mbaya; ni nzuri. Ni kama hiyo barabara imepata gorofa. Watu wanatembea chini ya gorofa lakini huko juu utendekazi na usafiri hujaanza. Wanakenya wengi wako katika giza, hawajui wakati barabara itaanza kutumiwa. Wengine wanasema kuna majumba yamejengwa ya kulipia pesa pale mbele. Sasa wanaulizana kama watatembea juu kwa Expressway ama chini. Haijulikani ni Wakenya wagani wataenda juu kwa malipo na wagani watatumia chini. Tunataka ufafanuzi kwa kina, vile Waingereza wanasema ‘in black and white’. Waweze kujua kama kweli Wakenya watakanyaga kule juu. Pesa ni ngapi italipwa kupitia kule juu? Na kama huna utafanya nini? Kazi ya ujenzi itakamilika lini? Isiwe ikawa Rais Uhuru Kenyatta amefanya kazi mzuri na hawezi launch ile kazi, ipitwe na wakati na kuzinduliwa na Serikali ijayo. Kama kazi ya ujenzi ingeisha na aizindue, kama vile Rais Mwai Kibaki alitengeneza Thika Superhighway na mpaka leo tukiitumia tunamkumbuka popote pale alipo. Na hakuna pesa unatozwa ukiwa unatumia barabara ile. Nimesikia tayari Wachina wanatengeneza vioski vya kulipa pesa ukitumia"
}