GET /api/v0.1/hansard/entries/1163747/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163747,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163747/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, unafahamu vizuri kuwa wakongwe ni mbegu na sisi ni mazao. Sisi tumetoka kwa wazee. Ikiwa tutaacha mbegu zetu vibaya, basi tutakuwa na jamii ambayo haina mwelekeo. Wengi wetu tulizaliwa na hao wakongwe. Wengine wetu tumebahatika kusoma. Wengine wetu ni Wabunge na wengine wanafanya kazi sehemu tofauti tofauti duniani. Baadhi ya watu wako nje ya Kenya. Ni vizuri kuangalia mbegu ambayo ilituleta. Mbegu hiyo ni wale wakongwe. Tukiwa na sheria mwafaka jinsi Hoja hii inavyopendekeza, basi sisi tutakuwa jamii ambayo inajali maslahi ya watu wasiobahatika na wakongwe ambao wako sehemu tofauti tofauti."
}