GET /api/v0.1/hansard/entries/1163753/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163753,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163753/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "ulipitisha sheria kuhusu wakongwe. Kwa hivyo, hutaweza kukataa. Wacha tujaribu kuitengeneza vizuri. Bw. Spika wa Muda, wewe ni mfugaji na ninajua kwamba wewe unajua maisha ya ufugaji vile inavyo kaa. Hebu angalia vizuri kama wewe ni mfugaji na umehama, na mzee leo hawezi hama na wewe, atakwambia mimi kichwa inaniuma, mara goti liko hivi. Kuna walemavu kadhaa ambao hawawezi kutembea kufika katika kituo cha pili mahali ambapo ng’ombe ama mbuzi zinaweza kuweka nanga zipate maji na nyasi. Itabidi wale ambao hawajabahatika kijamii wabaki katika sehemu ya mahame. Ukishawaacha katika hiyo sehemu ya mahame, basi utakua umepoteza watu muhimu. Kwa hivyo, mimi ninaona Sen. Nyamunga, alileta hii Hoja wakati mwafaka na inafaa itengenezwe na ipitishwe. Na pia, bunge za kaunti popote pale walipo, bunge tofauti tofauti, wanafaa wao pia wapitishe hizi sheria katika sehemu zao na pia watu hawa waangaliwe na watafutwe ili ministry ambayo inahusika isiwache wale wasio bahatika kijamii wawe wanateseka katika sehemu tofauti tofauti. Asante kwa kunipatia nafasi."
}