GET /api/v0.1/hansard/entries/1163757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163757,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163757/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "wengi sana; walikuwa 2,243 na nilikuwa na mtaji wao wa hela wa Kshs1 million ambao nilikua nawatunuku leo. Tumekuwa na msafara mkubwa sana Thika Road. Kwa hivyo, ni kweli kwamba nawania kiti cha Ubunge cha Ruiru na pia bado ninaongoza kwa kura ya maoni katika kiti cha Seneta wa Kaunti ya Kiambu. Ni jambo la kushangaza sana lakini nashukuru Mungu kwa jambo hilo. Hoja hii ambayo imewasilishwa Bungeni na rafiki yangu Sen. Nyamunga, ambaye anagombea kuwa Seneta aliyechaguliwa kule Kisumu, na pia ashawahi kua Mwakilishi wa akina Mama, ambaye tunashiriki kabisa katika maombi na pia tulikuwa katika jopo la maspika kama vile ulivyo hapa. Ni jambo nzuri sana ambalo ameliwasilisha hapa tukija katika kipindi cha lala salama cha Bunge la kumi na mbili ambayo ni Seneti ya pili ya Jamhuri ya Kenya. Watu wetu ambao ni wakongwe wameweza kutelekezwa kwa njia ambayo sio nzuri hata kidogo. Sio eti kusema kwamba kuna kutelekezwa ambako kunafaa; kama umetelekezwa ni kumaanisha kwamba hujatiliwa maanani. Fauka ya hayo, sisi sote tunaweza kua watahiniwa wakuwa vikongwe kwa miaka inayokuja. Kwa hivyo, wakati tunazungumzia Hoja hii ikumbukwe kwamba sio eti kwa sababu ni wale ambao tunawaangazia. Na ikumbukwe kuna kitabu cha aliyetuwacha, makataba mkange “Walenisi”, kwamba wale ni sisi. Ni sisi ambao tunahodhi hii nafasi baada ya miaka michache. Sasa ivi nimetoka kumuaga aliyekuwa Seneta Balozi (Dr.) Wilfred Machage tukiwa na Sen. Shiyonga na wengine tulio kuwa nao pale katika SDA Maxwell Church."
}