GET /api/v0.1/hansard/entries/1163759/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163759,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163759/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Amefariki akiwa na miaka 65 tu. Alikua mchanga sana. Katika hili Jumba kuna Maseneta wengi ambao wana umri ambao umefikia zaidi ya hapo. Kabla sijaendelea, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa jamaa na marafiki. Dr. Wilfred Machage tulijuana na yeye, na pia mtoto wake wa kwanza Steve Machage tulisoma na yeye Kenyatta University kutoka mwaka wa kwanza mpaka wa nne. Tumekuwa marafiki wa familia zetu mimi na mke wangu na mke wake, Mama Tema Mtupi, kutoka kule South Afrika. Kwa hivyo, ni watu ambao tumekua wa karibu kwa pamoja sana na wakati alipokua hapa alikua mmoja wapo ya jopo la maspika. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Kila mtu ana jukumu la kuweza kuwaangazia hawa vikongwe. Juzi tu nimempoteza nyanya yangu mpendwa akiwa na miaka 90. Kwa sababu mungu amenipatia uwezo nikawa Mbunge, angalau nilikua namsaidia kila mwezi namtumia pesa. Baada ya yeye kufariki, nilijiambia kwamba hizo hela hazina maana kwa sababu ningelipenda kuwa na yeye kwa muda mrefu. Sidhani kuna watu wengi wa umri huu wangu ambao watafikisha miaka hiyo 90. Mhe. Wario amesema tunachukua kemikali nyingi katika vyakula na hata kutoka katika mazingira ambayo tunaishi. Lakini kwa kweli kumekuwa na changamoto kubwa sana za kuweza kuwatunza wazee wetu. Kisa na maana ni kwa sababu, kitambo kidogo ilikua ni rahisi wawe kule vijijini alafu kama Isaac Mwaura akioa, atajenga kule, awe na wajukuu ambao watakua wakimliwaza nyanya au babu yao. Lakini sasa hivi sisi tumetorokea mijini na inabidi kwamba wakuu wetu wagure waje kukaa na sisi kwenye vyumba ambavyo ni vidogo sana, kwenye mazingira ambayo hayawapatii nguvu na wanaonekana kana kwamba ni bugdha kwa jamii. Wengi ambao pengine wamebarikiwa wana uwezo wa kuwajengea katika the"
}