GET /api/v0.1/hansard/entries/1163761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163761,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163761/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "lakini utakuta ya kwamba visehemu ambavyo tumejenga vyumba ni vidogo na wale ambao tayari wamepanga ama kukodisha katika hizi flats inakua ni vigumu sana kwa sababu nyanya atakaa kwenye sebuleni, hana pengine chumba cha kulala na kadhalika. Ni jambo ambalo tunafaa kuliangalia zaidi fauka tu ya kupatiana Kshs2,000 kila mwezi na matibabu ya National Health Insurance Fund (NHIF). Tujiulize, sera ile ambayo inafaa, sheria, nafikiri Mhe. Gathoni wa Muchomba amewasilisha sheria hii kule na Mhe. Cheruiyot alikua na nyingine hapa, ziweze kuwiana ili tuwe na sheria moja ya watu wazee ama ukipenda kwa kimombo, senior citizen, wakuu wetu ili waweze kulindwa kikamilifu na jamii. Haifai tu kuwa kwamba hilo liwe ni jukumu la Serikali kwa sababu, ikiwa ni mambo ya majukumu ya kiserekeli, itabidi basi tuweze kutengeneza mabweni ambapo hawa wakongwe wetu wataishi. Kama tunakumbuka, wakati tulikua tunaenda katika shule za malezi, unakuta kwamba kukaa katika haya mabweni ni mateso matupu. Hawa wakuu wetu wanahitaji kuwa wakiskia lile joto la kwamba wao wanaenziwa na familia zao, wanaweza kupata vichekesho na kadhalika. Mimi ni mwana bodi wa Leonard Cheshire Disability Services katika nchi hii ya Kenya ambayo ni mojawapo ya muungano wa Leonard Chesire International na tuko na nyumba za wazee kule Kariobangi, Huruma na kadhalika ambazo zinashughulikia hawa wazee. Ni changamoto kubwa sana kuwa na hela na uhakikishe kwamba hiyo miji inaendeshwa sawasawa isipokuwa ni wale watawa ambao wamejitolea kutoka kanisa la"
}