GET /api/v0.1/hansard/entries/1163764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163764/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Nafikiri ni muhimu tuangazie mambo ambayo tunaweza kutengeneza kama vile marupurupu ya uzeeni, mambo ya afya, na mambo mengine kama hayo. Kama ni ujenzi wa nyumba za wazee kwa sababu mara nyingi wanajenga nyumba zao wakati wanastaafu. Pengine pia kuwe na ushauri kama vile ambavyo nimeona imependekezwa hapa katika serikali zetu gatuzi ndiposa pia watu wazee waweze kujua kipato chao kitapungua, hawatakua na nguvu za mwili zitakazowawezesha wajikimu wenyewe. Bw. Spika wa Muda, ikumbukwe kwamba, hata mambo ya kukaa na wazazi mijini inawapendelea sana akina mama. Akina mama wanapendwa na watoto wao ambao huwaita mijini lakini wazee wanawachwa kule mashambani na ng’ombe zikilia na kutafuta majani. Mwanaume wa kiafrika ametengwa sana. Ameambiwa awe mkali kama simba kwa nyumba, akiguruma watu wote wanatorka. Hivyo hivyo, wanamtoroka akiwa mzee anabaki akiguruma peke yake huko kwa mashambani. Mara mama anaenda Marekani leo, kesho anaenda Mombasa na kwingineko. Mpaka mzee huyu wa miaka themanini anatafuta mtoto mdogo wa miaka kumi na tisa na kumuoa kwa sababu ya upweke. Bw. Spika wa Muda, haya mambo kama tutaangazia mimi na wewe na wengineo tutakwenda kwenye msururu huo huo. Nafikiri hatuna suluhu la kutosha na jambo hili haliwezi likakamilika kwa kupitia hoja hii. Ni muhimu tuweze kuifikiria kisheria na kijamii jinsi ya kutenga nafasi ya kuwasawazisha wazee wetu wajihisi kwamba wao pia ni wadau baada ya kufanyia Serikali na uma kazi na kujitolea kwenye jamii kwamba hawatawachwa nyuma eti kwa sababu sasa hawana maana kama vile watu wanafikiria umeshatumika, hauna nafasi katika jamii. Kwa hivo, kama Serikali zetu gatuzi, zingekuwa na mipango sambamba ambayo inajumuisha kile ambacho serikali ya kitaifa inafanya, itakuwa jambo nzuri sana ya kuvutia. Ningeomba pia wawe na idara maalum ambayo inashughulikia watu wakongwe ambayo itakua imefadhiliwa zaidi na imepatiwa pesa na bunge ya kaunti, ili waweze kushughulikia maswala haya. Pia kuwe na watabibu katika hospitali kuwe na vitengo maalum katika zile referral hospitals ambazo tumeziona zikijengwa kilakukicha, iili waweze kuwa wakisaidia wazee wetu wanaingia kule na wale tunaita Community Health workers (CHW) ambao wanafayanya kazi nzuri sana ili kuwapatia chanjo, madawa na kadhalika. Niliona vile nyanyangu aliteseka kabla ya kuiaga dunia. Pia, itabidi tuwe tunaajiri watu kwa nyumba hizo ambao kazi yao itakuwa kuwaangalia hawa wazee wetu. Kwa hivyo inafaa pia uwe hata na taaluma inayofunza jinsi ya kuwashughulikia wazee. Watu wafundiswe katika shule zetu hizi za teknologia, kuwe na mafunzo maalum ambayo wanafunza kwa sababu tuanendela kuzeeka na miaka inayokuja watu wengi watastaafu katika afisi za umma. Nadhania inakisiwa kwamba nusu ya wale ambao wameajiriwa sasa hivi ikifika mwaka wa 2025 watakua wakiondokea kazi zako. Wataenda wapi? Lazima tuanze kuangalia na hata kuwa na idara maalum katika serikali ya kitaifa na zengine katika serikali gatuzi ndiposa jambo hili lisiwe tu ni mzigo wa familia, watu ambao wa kipato cha chini kwa sababu uchumi umezorota na ndiposa pia tuweze kuwa na nguvu na uzoefu wa utaaluma."
}