GET /api/v0.1/hansard/entries/1163766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1163766,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163766/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Wakati nilikua naishi Uingereza, kulikua na majadiliano makubwa sana ya kwamba kuna watu ambao wamechukulia nyumba za wazee kama baishara na zilikua hata zinaweza kuwa na nafasi katika London Security Exchange . Can you imagine? Yaani watu wamefanya hio baishara kuwa kubwa mno hivi kwamba watu wanaweza kununua shares za kampuni hio kupitia London Security Exchange. Sisi pia tunafaa kufika pale. Hatufai kuwa tunatoza shida hii ya kijamii iwe ni kama ni biashara ya mtu kibinafsi. Tuuchukulie huu mzigo uweze kubebwa na familia kwa kiasi lakini serikali iwajibike ndiposa usiwe ni mzito sana, watu tuanze kuona kama vile tumeweza kuona huku mjini wakongwe wanaanza kuomba omba kwa barabara kwa sababu hawana chakula na wanaonekama wamedhoofika. Vile vile, mambo ya ulemavu yaangaliwe kwa sababu pindi unavyozeeka, ndivyo unazidi kuwa na ulemavu. Tunafaa kuangalia haya maneno na hata pia kupoteza fahamu na kuwa na upungufu wa akili. Haya ni mambo ambayo tunafaa kuyaangalia kwa makini ili kuhakikisha ya kwamba watu pia hawakuja na njia ambayo inaweza kujidhuru na tuwe tunaweza kujihami ya kutosha ndiposa tuweze kujali kila mtu ambaye atazeeka. Kwa hayo mengi, naunga mkono hoja hii na niombe kwamba iweze kupasishwa. Hoja hii isikuwe tu ni mapendekezo kama vile iko hapa. Sheria kabambe iwe, na kama zipo, ziweze kuhakikisha kama zinaweza kupitishwa kabala hatujafunga muhula huu wa mwisho ya Bunge la kumi na mbili. Naunga mkono. Asante sana."
}