GET /api/v0.1/hansard/entries/1163830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1163830,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163830/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya Taarifa kutoka kwa Seneta wa Nandi, Sen. Cherargei. Maombi aliyoyaleta hapa yanapaswa kuungwa mkono kwa sababu kwa muda mrefu, utalii wetu umekuwa ukiangazia masuala ya ufuo wa bahari na wanyama pori peke yake. Hatujatumia fursa ambayo tumepewa kujenga utalii wa michezo ambao pia ni muhimu. Tunaweza kuboresha sekta hii ili kuvutia wageni wengi kutembelea nchi yetu. Bi. Naibu Spika, tukiangalia sehemu kama vile Eldoret, Nandi na kote kule, kuna sehemu nzuri ambazo watalii ama wanamichezo hususan wale wanaokimbia masafa marefu; wanaweza kuchukua nafasi ya kuja kufanya mazoezi yao, huku wakitembelea nchi yetu ili tutapate fedha za kigeni. Bi. Naibu Spika, kule kwetu pwani kuna maeneo ambayo tunaweza kuwa na mchezo wa “ skiing.” Mchezo huu ni wa kuteleza katika mawimbi. Kwa Kiingereza tunasema wind surfing. Hii inaweza kufanyika kwa njia rahisi bila kuwa na gharama kubwa sehemu za Gongoni-Malindi hadi Lamu. Watalii wakiingia wanaposhuka Momabasa au Malindi, wanaweza kwenda kule na kufanya michezo yao halafu wanarudi makwao bila ya kuwa na shida yoyote. Taarifa hii imekuja wakati mzuri. Bi. Naibu Spika, jambo la mwisho, tunaweza kutumia jumba la Kenyatta International Convention Centre (KICC) kuvutia watalii wengi hapa nchini kwa kuimarisha michezo humo ndanio. Pia tunaweza kutumia viwanja vya Kasarani na Nyayo kuimarisha michezo mingi ambayo itawavutia watalii wengi hapa nchini. Tulipokuwa na World Cup mwaka wa 2004 kule Afrika Kusini, Kenya ilipoteza fursa adimu ya kuweza kukaribisha zile nchi ambazo zilikuwa zinakwenda huko. Wangeweza kufanya mazoezi yao ya kujitayarisha hapa. Wakati huo, hali ya hewa nchini Kenya hususan Mombasa ilikuwa sawa kuliko Afrika Kusini ambapo michezo hiyo ilikuwa inafanyika. Bi Naibu Spika, Taarifa hii itakuja kwa Kamati ya Utalii na Biashara. Tutaishughulikia ipasavyo. Ninaiunga mkono."
}