GET /api/v0.1/hansard/entries/1164817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1164817,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1164817/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Khaniri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 171,
        "legal_name": "George Munyasa Khaniri",
        "slug": "george-khaniri"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuungana na wenzangu kutoa rambirambi kwa mwendazake rafiki yangu mpendwa, Sen. (Dr.) Machage. Nilizipata habari za kifo cha Sen. (Dr.) Machage kwa masikitiko makubwa. Tumejuana kwa miaka mingi na kuna mengi ambayo tunashirikiana naye. Kwanza kabisa, vile mlivyosikia kutoka kwa Sen. Sakaja, tulienda kwenye Shule la Upili ya Chavakali, ingawa alikuwa huko miaka mingi mbeleni kabla yangu. Wakati mwingi tulipokuwa tukikutana, tulikuwa tukiongea kuhusu shule yetu ya zamani, Chavakali. La pili, tulifanya naye katika Bunge la Kitaifa akiwa Mbunge wa Kuria West nami nikiwa Mbunge wa Hamisi. Tukawa naye pia kama Mawaziri Wasaidizi katika Serikali ya Mhe. Kibaki. Hatimaye baadaye, tulijipata katika hili Bunge la Seneti akiwa Senata wa Migori nami nikiwa Seneta wa Vihiga. Kwa hivyo, yeye ni mtu ambaye ninaweza kusema kwamba tumetoka mbali. Tunamkumbuka kwa mambo mengi mazuri. Namkumbuka hasa kwa Kiswahili chake chema. Aliongea Kiswahili sanifu kabisa. Ndiyo maana niliamua siku ya leo niweze kutoa rambirambi zangu kwa lugha ambayo Sen. (Dr.) Machage aliipenda. Kiti chake katika Seneti kilikuwa ni hiki hapa nyuma yangu. Kwa utani, nilikuwa namwita, “ Bogi Benda.” Tukikutana ilikuwa ni, “ Bogi.” Kwa niaba yangu, familia yangu na watu wa Vihiga ninatoa rambirambi kwa familia yake, watu wa Migori na Kuria kwa kumpoteza kiongozi huyu shujaa. Natoa rambirambi zaidi kwa ndugu yake pacha ambaye walizaliwa pamoja, wakasoma pamoja na wakawa wote madaktari. Najaribu kufikiria yale huyo ndugu yake anaweza kuwa anayapitia sasa hivi kwa kumpoteza mtu ambaye walizaliwa pamoja na wamekuwa pamoja miaka hii yote mpaka katika uzee wao. Letu ni kusema Mwenyezi Mungu afariji jamii. Awapatie nguvu ya kustahimili msiba huu ambao umewapata. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Sen. (Dr.) Machage mahali pema mbinguni. Niruhusu pia nichukue wakati huu kutoa rambirambi kwa aliyekuwa Mbunge wa Mt. Elgon, Mhe. John Serut. Nilipata vile vile nafasi ya kufanya kazi naye katika Bunge la Kitaifa, akiwa Mbunge wa Mt. Elgon nami nikiwa Mbunge wa Hamisi. Tumesikia kwamba amekuwa mgonjwa kwa muda. Labda Mwenyezi Mungu amempumzisha. Tunaomba aiweke roho yake pahali pema mbiguni na aweze kufariji jamii ambayo ameiacha nyuma."
}