GET /api/v0.1/hansard/entries/1165253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165253,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165253/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Redio husikilizwa mahali pengi haswa humu nchini na ulimwenguni kwa jumla. Hapo awali, the Kenya Broadcasting Corporation (KBC) ndio ilikuwa stesheni ya radio pekee. Watu wengi walipenda kusikiliza the British Broadcasting Corporation (BBC), hususan habari za saa moja usiku na saa moja asubuhi ambapo tulikuwa tunapata ripoti za Kenya ambazo redio za Kenya hazikuzungumzia. Kwa hivyo, redio imetumika pakubwa kutoa habari na vile vile kuelimisha watu. Jana Sen. M. Kajwang’ alizungumzia kipindi cha shule katika miaka ya sabini ambacho kilikuwa kinaanza na wimbo; “Nilipokuwa kijana, nilicheza na masomo.” Wengi tulikuwa tunasoma wakati wa vipindi kama vile ambavyo vililetwa ili kuelimisha jamii kwa jumla na vile vile wanafunzi shuleni."
}