GET /api/v0.1/hansard/entries/1165255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165255,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165255/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, wenzangu waliotangulia wamezungumza kuhusu kutumika vibaya kwa redio. Ni kweli hapo awali redio imewahi kutumika vibaya. Hatungependa kurejea pale wakati huu ambapo tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi ambao utafanyika tarehe nane, mwezi wa nane, mwaka huu. Bi. Spika wa Muda, ni lazima chombo cha redio kitiliwe nguvu. Tumeona ya kwamba wasanii wengi wanaweza kutumia redio hizi ili kuleta sanaa zao, watu wajue na kuweza kuzinunua; yaani kupeleka sokoni sanaa zao. Lakini wengi hawalipwi. Utapata kwamba wale ambao wameweza kutunga nyimbo zao na mashairi yao na yakaweza kuchezwa katika redio hizi kwa sasa wanahangaika katika umaskini. Hawa wasanii wanatumia talanta zao kuleta nyimbo kama hizi ambazo watu wanaskiza kwa wingi; nyimbo zinachezwa kwa wingi katika redio na sehemu zingine lakini hawapati mapato kulingana na zile sanaa ambazo wameweza kufanya. Kwa hivyo, tunapoangalia maswala haya, tunapoadhinisha siku hii, ni wakati mwafaka wa kuweza kutafakari ni vipi tutaweza kusaidia talanta nyingi ambazo ziko katika kila jamii hivi sasa nchini Kenya. Ukienda kila mahali kwa sasa kama wewe ni mwanasiasa utatungiwa wimbo wa jamii ile ambayo unawakilisha au jamii ile ambayo ungependa kuwatumikia katika Bunge la Kaunti au Bunge la Kitaifa, Seneti ama ata Rais."
}