GET /api/v0.1/hansard/entries/1165257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1165257,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165257/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Talanta hii iko katika kila jamii na hivi sasa tumeona kwamba kuna redio nyingi za kitamaduni ama vernacular radios ambazo zinachukuwa fursa kubwa ya kuweza kuelimisha jamii katika maeneo yake. Lakini ningependa kuonya kwamba hizi redio za kitamaduni zisitumike kuchochea wananchi hususan wakati huu wa sasa ambao tunakwenda katika kura. Kwa sababu hiyo itavunja umoja wa nchi ambao sisi sote tunapigania tuwe na Kenya moja, tuwe watu wamoja ili sote tuweze kusonga mbele kimaendeleo. Kuliko kukigawanya nchi kikabila, sisi tuko kabila fulani, sehemu fulani, kwa hivyo sehemu hii haturuhusu mtu mwingine wa kabila nyingine kuja kusimama katika eneo letu na mambo kama hayo. Kwa hivyo, tupate fursa kwamba ile Media Council iwe macho hususan wakati huu wa sasa ambapo tunakwenda kwenye kura, kuhakikisha ya kwamba hizi redio za kienyeji hazitumiki vibaya katika mchakato wa kura. Asante Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii."
}