GET /api/v0.1/hansard/entries/1165774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165774,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165774/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika. Pia ningependa kuunga mikono Mswada huu wa kuelekeza uchumi bora ndani ya hizi kaunti zetu. Huu Mswada umekuja wakati unaohitajika. Mswada huu una mambo mengi ambayo tunaweza kufanya. Ninawapa kongole wale magavana wote sita walioanzisha mfumu huu wa uunganishaji wa kaunti sita za Pwani, kuanzia Lamu, Tana River, Kilifi, Mombasa, Kwale na Taita-Taveta. Magavana hawa walianzisha mfumo wa jumuiya zote sita za kaunti za Pwani. Pengine kwa bahati mbaya au kwa msukosuko au kwa kukosa kuelewana hii jumuiya ya kaunti za Pwani ilififia. Tuko na muda mdogo uliobaki wao kuwa katika mamlaka. Mswada huu sasa hivi uko ndani ya Bunge la Seneti. Ingefaa wafungue macho waelewe ya kwamba Mswada huu unaenda kusaidia kaunti zote sita za Pwani kwa muda mrefu sana. Ninampa kongole Sen. Nyamunga ambaye ni Seneta mteule wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kwa kuleta Mswada huu hapa, vile vile, kwa ukakamavu wake wa kujua mahitaji ya Mswada huu. Tunaelewa kabisa ya kwamba kama utafaulu ni lazima upate kielelezo mwafaka ambacho kitakuwa katika kilele cha utawala ya Jamhuri ya Kenya ili kuona ya kwamba haya yote tunayoyasema hapa, ambayo yapo kwenye Mswada huu, yatatekelezwa. Kutengeneza pesa ndani ya kaunti na Serikali ya Kitaifa, ni lazima ufisadi upigwe vita. Ikiwa hatutapiga vita ufisadi, basi itakuwa biashara kama kawaida. Tunajuwa yule atayegombea kiti cha urais na kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya ni “Baba” Raila Amollo Odinga. Yeye ndiye mtu tu anayeweza kupigana na ufisadi ndani ya Kenya kwa hivi sasa. Hii ni kwa sababu anajuwa pale matunda ya ufisadi yako na anaweza kuyaziba sawasawa ili kuona kwamba kaunti zote 47 zinafaidika."
}