GET /api/v0.1/hansard/entries/1165776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165776,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165776/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Hii si ndoto bali ni kwamba Mswada huu unaweza kutekelezwa. Hivi sasa macho ya kaunti zote 47 yanaelekeza katika Serikali ya Kitaifa ambayo imekuwa ikisaidia kaunti kwa kuzipelekea pesa. Hizi pesa tunazopigania hapa tukizipeleka, ingekuwa serikali zetu za mashinani ziko na utaratibu wa kutafuta pesa zao ziongezee juu ya hizo, zingeweza kuleta maendeleo mengi sana. Ninasisitiza kwamba hakuna kaunti kati ya zile 47 ndani ya serikali ambayo haina kitega uchumi. Tukianzia mambo ya utalii, tuko na mbuga za wanyama, bahari, upeo mzuri sana katika kila mahali, tukianza na upande wa Pwani. Nchi nyingi katika ulimwengu zimeweza kufaidika kwa sababu ya utalii. Kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River na hata Lamu zinaweza kuendelea zaidi ikiwa serikali zao zitaweka akili pamoja na kutafuta ni kitega uchumi ambacho wanaweza kufaidika nacho."
}