GET /api/v0.1/hansard/entries/1165780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1165780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165780/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Singapore ni nchi ndogo, lakini kwa sababu iko na ports imefanya maajabu. Ukienda kule watu wamefaidika na uchumi wa nchi yao. Singapore inajulikana kwa sababu iko na bandari. Bandari peke yake inafaidi kila mtu Singapore. Sisi hapa tuna bandari na hatujui pale ilipo kwa sababu inasaidiwa pia na Serikali. Tunashindwa kama bandari ya kule Singapore inaweza kusaidia serikali. Yetu hapa ni kinyume kwa sababu ya ufisadi. Jiji la Mombasa likiwa na bandari kama Singapore City, watu wa kwanza kufaidika na ile bandari ni wakaaji wa Mombasa. Tukiangalia uchumi wetu na hali yetu ya Maisha, ukifika Mombasa sasa hivi utaionea huruma. Imekuwa gofu; watu wamepoteza kazi na hakuna kitega uchumi. Imeachiliwa tu. Ikiwa tunataka Kaunti ya Mombasa iendelee mbele, ni lazima wapewe nafasi ya kuendesha na kuangalia ni asilimia ngapi watakaopata kutoka kwa bandari ili Mombasa iweze kuendelea. Mombasa, ambayo ni kama mama yetu, ikiendelea tuna hakika uchumi ndani ya Pwani, kuanzia Kilifi, Tana River, Lamu, Kwale, Taita-Taveta watafaidika. Kwa hivi sasa, hili ni jambo la kusikitisha."
}