GET /api/v0.1/hansard/entries/1165784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1165784,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165784/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kuna Sharja na hizo zingine ambazo ndugu yaki, Sen. Faki, amesema kama vile Abu Dhabi. Bi. Naibu Spika, hakuna mtu anaweza kuishi pekee yake. Ukienda Sharja, Dubai na pande zingine utapata kama nilivyotangulia kusema, ukiwa unapeleka gari kule, ukija huku kwingine petroli iko sawa sawa. Kuna usawa pia katika maendeleo ya pande zote. Nilikua natazama video ya mtaalam mmoja kutoka United States of America (USA) na alikua anashangaa. Alisema, ‘ you did this in 50 years ?’ Katika miaka 50 wamegeuza United Arabs Emirates (UAE) ikakua kitu ambacho ulimwengu mzima unashangaa. Kila kitu kinafanya kazi kisawasawa. Hiyo inamaanisha kwamba UAE zinafanya kazi pamoja. Mswada huu unaweza kutuunganisha sisi na kufanya Kenya ikawa moja. Mswada huu unaweza saidia Wakenya kupendana. Leo tumekaribia uchaguzi na tumeanza kutengana kikabila. Tumeanza kupanga kisiasa makabila fulani yakusanyike ili yapige kura. Haipaswi kuwa hivyo. Sisi wote ni Wakenya. Kama vile Sen. Sakaja husema, hakuna Kenya A ama B. Ni ukweli kwamba Kenya iliyoko ni moja. Kwa hivyo, sisi wote ni Wakenya na lazima tusikizane. Kama kaunti zote 47 zingekuwa zinaelewana, pengine hatungehitaji Mswada huu. Lakini, tunauhitaji kwa sababu ya uelekezo kwa wanaosema lazima kaunti ziwache kutegemea Serikali ya Kati kupata pesa. Wao wenyewe wawe na mikakati yao katika serikali za kaunti na waketi huko; sio kuketi na kungoja pesa tunazopeleka ili ziingie kwenye mifuko yao binafsi. Mswada huu utendeke hili uweze kusaidia Wakenya kokote wanaokoishi katika nchi. Swala la mwisho ni kuwa kule Pwani kuna kitega uchumi katika pande ya Kwale ambacho hakijapewa nguvu na Serikali. Tunaweza kutengeneza sukari. Sukari nyingi inaletwa kutoka nchi za nje. Hii nchi iko na uwezo na ardhi ya kutengeneza sukari. Lakini mambo ya ufisadi yameingia katika uzalishaji wa sukari hadi makampuni yamekufa. Ramisi Sugar iko Kaunti ya Kwale. Inatakikana ipewa kipau mbele na serikali ya Kaunti ya Kwale ili isifungwe na watu wakapoteza kazi. Pande za Nyanza, Mumias Sugar na Nzoia Sugar wamepoteza rasilimali zao za upandaji wa miwa. Bi. Naibu Spika, ni jambo la kusikitisha tukitazama kwamba nchi ambayo inaweza kutengeneza sukari haina kampuni. Siku zote, sukari ikona shida, ilhali iko katika majimbo ya Nyanza na Western ambayo yakishikana, yatatengeneza sukari nyingi. Kampuni ingine ni Ramisi Sugar lakini hakuna masikizano. Huu mmea wa miwa umezidi kudidimia. Mswada huu ukipitishwa tutahitaji ushirikiano mwema katika Kaunti zote 47."
}