GET /api/v0.1/hansard/entries/1165788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1165788,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165788/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu kuhusu uimarishaji wa rasilimali za kaunti ambao umeletwa Bungeni na Sen. Nyamunga ambaye ni Seneta Maalum. Nadhani Mswada huu umekuja wakati mzuri, japokuwa kulingana na malengo na maazimio yake, ulifaa kupitishwa miaka saba au nane iliyopita, kwa sababu kwa sasa kaunti zetu nyingi zinategemea mgao wa Serikali ili kuendesha miradi yao ya maendeleo. Maendeleo inaweza kufanywa kwa msaada; maendeleo inatakikana kufanywa na rasilimali za kaunti ambazo zinapatikana katika eneo hilo. Mswada huu utasaidia pakubwa kuziwezesha kaunti zetu kuangalia zaidi rasilimali walizonazo kuliko kuomba Seneti kuwaongeza pesa kila mwaka ilhali wana rasilimali za kutosha kuhakisha kwamba wanapata pesa za kuendesha mipango na miradi yao. Kwa mfano, katika Mwaka wa Fedha 2020/2021, Kaunti ya Mombasa ilipokea zaidi ya Kshs7 billioni kutoka kwa Serikali ya Kitaifa. Walitarajia kukusanya Kshs6 billioni lakini walikusanya Kshs3.3 billioni. Hiyo ni karibu nusu. Hawakuweza kukusanya nusu ya matarajio yao ya fedha ambazo walitakikana kukusanya. Kama tunavyojua, Serikali ya Kitaifa ina mahitaji mengi. Kwa hivyo, kila mwaka, ruzuku ambazo zinatolewa kwa kaunti zetu zinazidi kupungua kwa sababu mahitaji yamekuwa mengi. Mapato pia yanaweza kupungua kutokana na uchumi kuzorota. Ikiwa rasilimali ambazo ziko katika kaunti zetu zitaimarishwa, ina maana kwamba kaunti itaweza kukusanya pesa nyingi za kodi. Hiyo itazuia watu kuhamahama kutoka maeneo ya mashambani kwenda mijini. Wengi wanatoka mashambani kwenda mijini kwa sababu hakuna kazi mashambani. Pia itapunguza umaskini. Ikiwa wale walioko mashambani watakuwa wanapata kazi kule, mtu hataona haja ya kuhamia mjini kwenda kulipa kodi nyingi. Maisha ya mjini pia ni ghali zaidi kuliko ya mashambani. Hii itasaidia pakubwa kupunguza umaskini katika kaunti zetu. Hali hii inaingiana na lengo la serikali inayotarajiwa ya Azimio la Umoja ambalo ni kuhakikisha kwamba maendeleo inaenda mashinani. Lengo na madhumuni ya ugatuzi ilikuwa kuleta serikali na vile vile maendeleo karibu na wananchi. Zamani maendeleo yote ilikuwa inapangwa kutoka Nairobi. Sasa hivi, kila kaunti ina fursa ya kupanga maendeleo yake. Inamaanisha kwamba kaunti nyingi zitaweza kuendelea pakubwa iwapo Mswada huu utapitishwa na kuwa sheria. Mswada huu unaangazia kuwepo kwa regional economic blocs, yaani jumuia za kaunti zilizoko maeneo fulani. Kwa mfano, katika eneo la Pwani, kuna kaunti za Lamu, Mombasa, Tana River, Kilifi, Kwale na Taita-Taveta. Zamani, kaunti hizo zote zilikuwa katika Mkoa wa Pwani."
}